[IRP] 10 IRP -Swahili version

Grace Mutung'u Bomu nmutungu
Wed Mar 30 23:25:15 EEST 2011


Dear All,
Please find as inline text,
Cheers!

*HAKI NA KANUNI 10 ZA MTANDAO WA INTERNET
*
Hati hii inafafanua haki na kanuni kumi muhimu ambazo ni msingi kwa uongozi
bora wa Mtandao wa Internet (Mtandao). Zimekusanywa na Muungano wa Haki na
Kanuni za Mtandao *(Dynamic Coalition on Internet Rights and
Principles),*ambao ni mkusanyiko wazi wa watu binafsi na mashirika
yanayozingatia haki za
kibinadamu katika Mtandao. Kanuni hizi zinazingatia viwango vya haki za
kibinadamu vya kimataifa na zimetokana na Mkataba wa Haki na Kanuni za
Mtandao ambao unatengenezwa na muungano huu.Mtandao umetoa fursa ya kipekee ya utambuzi wa haki za kibinadamu. Pia
jukumu lake katika maisha yetu ya siku kwa siku linaendelea kuongezeka.
Hivyo, ni muhimu kwa wahusika wote, umma na binafsi, kuheshimu na kulinda
haki za kibinadamu kwenye Mtandao. Hatua pia lazima zichukuliwe ili
kuhakikisha kwamba vile ambavyo Mtandao unatumika na kuzidi kukua, haki za
kibinadamu zinatekelezwa kwa kiasi kikubwa iwezekanavyo. Kwa minajili ya
kuafikia maono haya ya Mtandao ambapo haki za kibinadamu zinatimizwa, haki
na kanuni 10 za Mtandao ni:1) Kupatikana Kote na Usawa
Binadamu wote wamezaliwa huru na sawa kwa hadhi na haki ambazo lazima
ziheshimiwe, zilindwe na kutimizwa kwa mazingira ya Mtandao.2) Haki na Uadilifu kwa Jamii
Mtandao ni fursa ya kukuza, kulinda na kutekeleza haki za kibinadamu na
maendeleo ya uadilifu katika jamii. Kila mtu ana wajibu wa kuheshimu haki za
binadamu wengine wote katika mazingira ya Mtandao.


3) Upatikanaji
Kila mtu ana haki sawa ya kupata na kutumia Mtandao salama na wazi.

4) Kujieleza na Kujiunga
Kila mtu ana haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari kwa uhuru kwenye
Mtandao bila udhibiti au kuingiliwa. Kila mtu pia ana haki ya kujiunga kwa
hiari kupitia na kwenye Mtandao, kwa madhumuni ya kijamii, kisiasa,
kitamaduni au sababu nyingine.

5) Faragha na Ulinzi wa Takwimu
Kila mtu ana haki ya faragha akiwa Mtandaoni. Hii inajumuisha uhuru wa
kutofuatiliwa, haki ya kutumia msimbo (encryption), na haki ya
kutokujitambulisha Mtamboni. Kila mtu pia ana haki ya ulinzi wa takwimu,
ikiwa ni pamoja na udhibiti wa ukusanyaji wa takwimu binafsi, uhifadhi,
usindikaji, uondoaji na utoaji taarifa.

 6) Maisha, Uhuru na Usalama
Haki za maisha, uhuru, na usalama lazima ziheshimiwe, zilindwe na zitimizwe
Mtandaoni. Haki hizi lazima zisikiukwe,au kutumiwa kukiuka haki zingine
katika mazingira ya Mtandao.


7) Utofauti
Utamaduni na lugha mbalimbali kwenye Mtandao lazima kukuzwa, na ufundi na
ubunifu wa sera lazima zitiliwe maanani ili kuwezesha uwepo wa wingi wa
kujieleza.

8) Usawa wa Mitandao
Kila mtu ana haki ya kufungua kupata maudhui ya Mtandao kote, bila ubaguzi
kipaumbele, kuchujwa au kudhibiti trafiki kwa misingi ya kibiashara, kisiasa
au mengine.

9) Viwango na Taratibu
Usanifu wa Mtandao, mifumo ya mawasiliano, hati na jinsi za takwimu katika
Mtandao zitatengenezwa kwa viwango vya wazi ili kuhakikisha utangamano
kamili, ushirikishaji na fursa sawa kwa wote.

 10) Uongozi Bora
Haki za kibinadamu na uadilifu wa kijamii lazima ziwe kwenye misingi ya
utawala na sheria za utumizi na uongozi wa Mtandao.  Hii itakuwa kwa njia ya
uwazi, ushirikishaji wa mataifa, ujumuishaji na uwajibikaji.

Jihusishe na kuendeleza Mkataba wa IRP sasa kwa kwenda kwa anwani *
www.irpcharter.org*, Tufuate katika @ *netrights* kwa *Twitter* au ujiunge
na kundi la Haki na Kanuni za Mtandao *(Internet Rights and Principles)*kwenye
*Facebook*

-- 
Grace L.N. Mutung'u (Bomu)
Kenya
Skype: gracebomu
Twitter: GraceMutung'u (Bomu)
-------------- next part --------------
An HTML attachment was scrubbed...
URL: <http://lists.internetrightsandprinciples.org/pipermail/irp-internetrightsandprinciples.org/attachments/20110330/11304d21/attachment.htm>More information about the IRP mailing list